News
Rais Xi Jinping wa China ashiriki sherehe ya kuadhimisha miaka 25 tangu Macao irejee China
Rais Xi Jinping wa China ameshiriki kwenye sherehe ya kuadhimisha miaka 25 tangu Macao irejee China katika Jumba la Michezo la Asia Mashariki la Macao usiku wa jana Alhamisi, na pia atashiriki kwenye hafla ya kuapishwa kwa serikali ya awamu ya sita ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao (SAR) na kufanya ziara ya ukaguzi mkoani humo.
Rais Xi na mkewe Bi. Peng Liyuan waliingia kwenye ukumbi wa sherehe wakiambatana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Macao, Bw. He Yicheng na mkewe Zheng Suzhen, na kupokewa kwa makofi ya furaha. Walitazama tamasha lenye maonyesho mbalimbali yakiwemo uimbaji wa nyimbo, ngoma na muziki. Mwishoni mwa tamasha hilo, rais Xi alijiunga na watazamaji kuimba kwa pamoja "Hongera Nchi Mama", akiitakia China ustawi na mkoa wa Macao mustakabali mzuri zaidi.